IQNA

Maonyesho ya ustaarabu wa Waislamu yafunguliwa Marekani

11:01 - May 30, 2011
Habari ID: 2130476
Maonyesho ya ustaarabu wa Waislamu yamefunguliwa Mei 27 na yataendelea kwa miezi saba katika Kituo cha Sayansi cha California huko Los Angeles.
Maonyesho hayo yenye anwani ya ‘Uvumbuzi 1001’ yako katika mzunguko wa miaka mitano duniani na tayari yameshafanyika London, Istanbul na New York.
Maonyesho hayo yanaangazia mchango wa wanawake na wanaume katika Kipindi cha Dhahabu cha Ustaarabu wa Kiislamu. Wanaotembelea maonyesho hayo wataona mchango wa Waislamu kuhusu fani mbalimbali za tiba, fizikia, ubaharia, usanifu majengo na hesabati.
Maonyesho hayo yanaonyesha mafanikio ya wanasayansi Waislamu kutoka eneo linaloanzia Uhispania hadi China kuanzia karne ya 7 hadi 17 Miladia.
800085
captcha