IQNA

Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani kwa watoto wa Misri

18:31 - May 30, 2011
Habari ID: 2131105
Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa watoto wa Misri walio na umri wa chini ya miaka minne yanaendelea katika mji wa Alexandria nchini humo.
Mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri. Akizungumzia suala hilo Muhammad Wahdan Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Uhubiri ya Idara ya Wakfu ya Alexandria amesema kuwa mashindano hayo yaliyoanza mwanzoni mwa wiki hii yataendelea hadi Alkhamisi tarehe 16 Juni. Amesema watoto kutoka sehemu mbalimbali za mji huo watashindana katika makundi manne ya kuhifadhi Qur'ani nzima, hifdhi ya thuluthi tatu za Qur'ani, hifdhi ya juzuu 15 za Qur'ani na hatimaye hifdhi ya juzuu saba za kitabu hicho kitakatifu.
Wahdan amesema kuwa kamati maalumu ya waamuzi na wataalamu wa Qur'ani wakiwemo maimamu wa misikiti ndiyo itakayosimamia mashindano hayo. Amesema washindi wa mashindano yaliyotajwa watapata fursa ya kwenda kuhiji mjini Makka. 800767
captcha