IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Britain kufanyika Wales

18:26 - May 30, 2011
Habari ID: 2131116
Awamu ya mwisho ya mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Britani (Britain) makhsusi kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu yamepanga kufanyika tarehe 17 hadi 19 Juni katika Chuo Kikuu cha Cardiff huko Wales.
Kituo cha habari cha FOSIS kimeripoti kuwa duru ya mwisho ya mashindano hayo yanayosimamiwa na Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Wanachuo (FOSIS) itafanyika pambizoni mwa kongamano la 48 la kila mwaka la jumuiya hiyo.
Wasomaji Qur'ani walioshiriki katika awamu za utangulizi za mashindano hayo yaliyofanyika kote Britani ndio watakaochuana katika awamu hii ya mwisho.
Kitengo cha mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kina sehemu tatu za hifdhi ya juzuu ya 30, hifdhi ya suratul Baqarah na hifdhi ya sura za kuanzia Fatiha hadi al An'am au kuanzia Yasin hadi surat Nas.
Katika upande wa kiraa, washindani watachagua sura mbili kati ya sura za Rahman, Hasr, Mulk, Muzammil, Qiyama na sura nyingine moja kati ya Yusuf, Ibahim, Yasin, Qaf na Waqia' kwa kutilia maanani sheria za tajwidi.
Kongamano la 48 la kila mwaka la Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Britani litafanyika katika siku za tarehe 17 hadi 19 Juni kwa anwani ya "Rangi Moja za Uislamu". Kongamano hilo litahutubiwa na wasomi wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani. Vilevile kutakuwepo maonyesho, warsha za mafunzo na mashindano mbalimbali ya Kiislamu.
Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Wanachuo wa Britain (FOSIS) uliundwa mwaka 1963 kwa shabaha ya kutetea na kulinda taasisi na jumuiya za Kiislamu za vyuo na taasisi za elimu ya juu. 801094


captcha