Habari zinasema kuwa walowezi hao wa Kizayuni waliandamana na viongozi wa kidini wa Kiyahudi wakisindikizwa na askari wa Israel katika mashambulizi hayo yaliyofanyika saa saba usiku wa kuamkia leo dhidi ya kaburi tukufu na Nabii Yusuf (as).
Askari wa utawala ghasibu wa Israel waliweka kizuizi katika eneo la Hawarah na kuzuia Wapalestina kuingia katika eneo hilo. Magari 50 ya kijeshi yaliandamana na walowezi hao katika kushambulia kaburi la Nabii Yusuf na kulikalia kwa mabavu eneo hilo takatifu hadi saa 11 asubuhi. 801031