IQNA

Mpango wa Wazayuni wa kubadilisha muundo wa Quds Tukufu

12:48 - May 31, 2011
Habari ID: 2131417
Utawala ghasibu wa Israel umezindua mpango mchafu wa kuuyahudisha mji wa Al Aqsa na kubadilisha muundo wake wa idadi ya watu kwa kisingizio cha kuimarisha uchumu wa mji huo.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza azma yake ya kutoa bajeti ya milioni 80 US$ za kutekeleza kile kinachotajwa ni 'mpango kamili ya kiuchumi' katika kipindi cha miaka mitano.
Mpango huo ambao Wapalestina wanasema ni kuendeleza sera za kuuyahudisha mji wa Quds, unajumuisha utekelezwaji miradi kadhaa na kuhimiza Wazayuni kuhamia hapo.
Imetangazwa kuwa milioni 42 US$ zitatumika katika kustawisha miundo mbinu katika Ukuta wa Magharibi (Ukuta wa Buraq).
Wizara ya Utalii ya Utawala wa Kizayuni imesema pia itatumia dola millioni 21.5 kuhimiza ujenzi wa hoteli na kupanua zilizopo. Aidha Wazayuni wanatumia millioni 20.5 US$ kaunzisha vituo vya utafiti huku milioni 20.26 US$ zikitumika kujenga mabweni.
Wanaharakati wa Kiislamu na Kisiasa wa Palestina wametoa wito kwa jamii ya kimataifa hasa nchi za Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za kivitendo kuwazuia Wazayuni katika njama zao za kuuyahudisha mji wa Quds ambao ni Qibla cha kwanza cha Waislamu.
801214
captcha