Msikiti huo ulio katika mji wa Edirne kaskazini-magharibi mwa Uturuki ulijengwa katika kipindi cha kati ya mwaka 1568-1574 Miladia. Ulijengwa na Khaje Mi’mar Sanan Agha kwa amri ya Sultan Selim wa Pili wa silisili ya watawala wa Kiuthmaniyya.
Baada ya Msikiti wa Divrigi, Msikiti wa Selmiya ndio msikiti mkubwa zaidi nchini Uturuki kuwekwa katika orodha ya turathi za dunia. Msikiti huo ni kazi bora ya usanifu majengo wa Khaje Mi’mar Sanan Agha ambaye alikuwa msanifu majengo rasmi wa Ufalme wa Uthmaniyya wakati wa utawala wa Masultani kadhaa.
Msikiti wa Selmiye vile vile una shule, hospitali, maktaba na bafu ya umma. Aidha una madrasa ya kidini ijulikanayo kama Darul Hadith, ukumbi wa kukadiria saa na soko ndogo. Msikiti huo una muundo wa oktagoni na una nguzo nane.
Kamati ya turathi za dunia ya UNESCO itatangaza orodha mpya ya turathi za dunia Juni 19
801169