Warsa hizo zitatoa muongozo wa kitaalamu kwa vituo vya kujifunza Qur’ani katika masuala yanayohusu uendeshaji, ushauri, mafunzo na utafiti.
Shirika la Qatargas limesema kufadhili harakati za kielimu ni moja ya malengo yake ya kutoa msaada kwa jamii. Afisa wa shirika la Qatargas Bw. Al Naimi amesema shirika hilo linafungamana na suala la kutoa ufadhili katika sekta za elimu, afya, na michezo kote Qatar.
Akishukuru Qatargas kwa msaada wake afisa mwandamizi wa Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu nchini Qatar Dr. Al Ibrahim amesema kuwa kufunza na kusoma Qur’ani Tukufu ni kati ya thamani za kijamii na kiutamaduni za Qatar.
Mpango huo wa Qatargas unafanyika chini ya anuani ya ‘Nyumba ya Qur’ani’ na unasimamiwa na Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu Qatar na ushirikiano na wataalamu kadhaa.
801794