IQNA

Maonyesho ya ‘Mimiea katika Qur’an na Hadithi za Mtume’

14:05 - June 02, 2011
Habari ID: 2132709
Maonyesho ya mimea iliyotajwa katika Qur’ani Tukufu na Hadithi za Mtume SAW yanafanyika katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Sharq, maonyesho hayo yaliyofunguliwa wiki iliyopita yataendelea hadi Julai 5.

Maonyesho hayo ya Bustani la Qur’ani la Qatar yamewasilishwa kwa umma ambapo kuna maelezo kwa lugha mbili za Kiarabu na Kiingereza kuhusu faida za kitiba za mimea hiyo.
Bustani ya Qur’ani ndiyo ya kwanza ya aina yake Qatar na inajumuisha mimeia yote iliyotajwa katika Qur’ani, Sunna na Hadithi za Mtume SAW.
Aidha kuna maelezo kuhusu mimea hiyo kwa msingi wa sayansi za kisasa. Bustani ya Qur’ani Qatar ilianzishwa Septemba 2008 na Taasisi ya Sayansi, Elimu na Maendeleo. Ni sehemu ya kipekee kwa wasomi na wanafunzi wanaofanya utafiti kuhusu tiba ya mimea.
802209
captcha