IQNA

Fainali ya mashindano ya Qur'ani kufanyika Mwezi wa Ramadhani

14:22 - June 06, 2011
Habari ID: 2133688
Fainali ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya Morocco itafanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mashindano hayo yenye anwani ya 'Mashindano ya Mfalme Mohammad' yanajumuisha hifdhi, qiraa ya tarteel na tajwid na yatafanyika katika Msikiti wa Al Sunna katika mji mkuu Rabat kuanzia Agosti 13 hadi 15. Hayo ni kwa mujibu wa Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu Morocco.
Wizara hiyo imetangaza kuwa mashindano ya mchujo yalifanyika katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ushirikiano na idara za kielimu za kieneo.
803221
captcha