IQNA

Qur'ani Tukufu kusomwa katika makanisa ya Marekani

15:16 - June 06, 2011
Habari ID: 2133756
Maqari wa Qur'ani Waislamu wanatazamiwa kusoma kitabu hicho kitukufu katika makanisa ya Marekani sambamba na maadhimisho ya Siku ya Milango Wazi na Makanisa nchini Marekanihapo tarehe 26 Juni.
Kituo cha habari cha Saphirnews kimeripoti kuwa Siku ya Milango Wazi ya Makanisa kwa ajili ya Waislamu na Wayahudi wa Marekani imeandaliwa na jumuiya ya Muungano kati ya Dini Mbalimbali na taasisi ya Human Rights First kwa lengo la kunyanyua juu utamaduni wa mazungumzo na kutayarisha uwanja mzuri wa kutambuana wafuasi wa dini za mbinguni.
Moja ya malengo ya Siku ya Milango Wazi ya Makanisa nchini Marekani limetajwa kuwa ni kupambana na propaganda za kuuchafulia jina Uislamu, kukiarifisha kitabu kitakatifu cha Qur'ani kupitia qiraa ya makari mashuhuri na kukabiliana na njama zinazopangwa dhidi ya Uislamu. Watayarishaji wa Siku ya Milango Wazi ya Makanisa pia wanapanga kutayarisha Siku ya Milango Wazi ya Misikiti ambapo Mamarekani Wakristo na Wayahudi wataalikwa kutembelea misikiti ya Wislamu. 803679
captcha