IQNA

Kamati ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani na Hadithi yabuniwa Kuwait

14:04 - June 07, 2011
Habari ID: 2134213
Kamati kuu ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani na Hadithi maalumu kwa vijana wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi imebuniwa nchini Kuwait.
Kamati hiyo imebuniwa chini ya uenyekiti wa Jasim Ya'qub Naibu Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Vijana na Michezo ya Kuwait.
Mashindano hayo yamepangwa kufanyika nchini humo tarehe 25 hadi 29 Septemba.
Kamati hiyo itatekeleza majukumu yake katika fremu ya ratiba ya kamati ya vijana ya sekretarieti ya baraza lililotajwa ya mwaka 2010-2011. 804034
captcha