Kwa mujibu wa gazeti la Ash-Sharq, mpango huo ujulikanao kama Quras umeandaliwa na kitengo cha wanawake cha Idara ya Kuhifadhi Qur’ani cha Taasisi ya Misaada ya Ash Sheikh Eid.
Mkurugenzi wa idara hiyo amesema mpango huo ni maalumu kwa wanawake na kila anayetaka kushiriki ni sharti awe amehifadhi kwa uchache juzuu mbili za Qur’ani.
Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kustawisha kiwango cha kuhifadhi Qur’ani miongoni mwa wanawake na kuwahimiza kuendeleza harakati za kuhifadhi Qur’ani.
803811