IQNA

Agosti Mosi siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani Kuwait

19:28 - June 08, 2011
Habari ID: 2135163
Adil al-Marzouq, mtaalamu wa masuala ya nujumu wa Kuwait amefanya uchunguzi unaoonyesha kwamba tarehe Mosi Agosti ndiyo itakayokuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1432 Hijiria.
Akibainisha zaidi suala hilo, al-Marzouq amesema kuwa Ramadhani ya mwaka huu itakuwa na siku 29 na kwamba kuonekana hilali ya kuanza mwaka huu kutakuwa kugumu katika hali ambayo hilali ya Idul Fitr itaonekana kirahisi iwapo hali ya hewa itakuwa nzuri.
Mtafiti huyo wa Kuwait amesema kuwa jua la siku ya kabla ya kuanza mwezi wa Ramadhani litatua saa moja na dakika moja kwa wakati wa mji mtakatifu wa Makka na kwamba hilali itaonekana karibu dakika 20 kabla ya kutua jua hilo. Amesema kwa vile kuonekana hilali katika usiku wa kuamkia mwezi wa Ramadhani kutakuwa kugumu, mwezi wa Shaaban utakuwa na siku 30 na mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanza siku ya Jumatatu.
Ameongeza kuwa hilali ya mwezi wa Shawwal itaonekana saa kumi na mbili na dakika nne alfajiri kwa wakati wa Kuwait siku ya Jumatano tarehe 31 Agosti, ambayo itakuwa sawa la Shawwal Mosi. 805504
captcha