IQNA

Kikao cha pili cha mfumo wa benki wa Kiislamu chaanza Singapore

13:32 - June 09, 2011
Habari ID: 2135292
Kikao cha pili cha kimataifa cha mfumo wa benki wa Kiislamu kilianza jana Jumatano huko Singapore.
Kwa muibu wa tovuti ya Zawya, zaidi ya wataalamu na wawakilishi wa mashirika ya kifedha na benki wapatao 450 kutoka kila pembe ya dunia wanashiriki katika kikao hicho kwa shabaha ya kuchunguza matatizo, changamoto na njia za kuimarisha nafasi ya uchumi wa Kiislamu katika kunyanyua kiwango cha ushirikiano miongoni mwa taasisi za kibiashara na kiuchumi duniani.
Kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Taasisi ya Fedha ya Singapore, kimefunguliwa kwa hotuba ya Lim Hng Kiang, Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchi hiyo.
Ustawi wa uchumi wa dunia ni jambo jingine ambalo linajadiliwa katika kikao hicho ambacho kimepangwa kumalizika leo Alkhamisi. 805515
captcha