Mshauri wa Masuala ya Utamaduni katika Kituo cha Masuala ya Misikiti Tehran Hujjatul Islam Ezatollah Vaezi amesema misikiti 500 Tehran itaandaa ibada ya I’tikafu.
Amesema usajili ulianza wiki mbili zilizopita na utaendelea hadi tarehe 12 Rajab (15 Juni) siku moja kabla ya ibada hiyo ya I’tikafu kuanza.
Amesema kuna ongezeko kubwa la wanaotaka kushiriki katika ibada ya I’tikafu mwezi wa Rajab kiasi kwamba baadhi ya misikiti haiwezi kumudu idadi kubwa ya waumini.
Mwaka jana zaidi ya watu laki saba wengi wao wakiwa vijana walishiriki katika ibada hiyo.
I’tikafu ni ibada ambayo hujumuisha kubakia katika msikiti kwa muda fulani kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
805348