Abdoulaye Wade ameidhinisha pendekezo la Ahmad Muhammad Ali Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kiislamu la kuanzisha Benki ya kwanza ya Waqfu nchini Senegal.
Muhammad Ali alitoa pendekezo hilo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Maualamaa wa Kiislamu hivi karibuni mjini Dakar.
Alisema hatua hiyo inalenga kueneza uwekezaji katika masuala ya misaada na kuwasaidia masikini.
Rais wa Senegal amesema Benki ya Maendeleo ya Kiislamu na taasisi nyinginezo za Kiislamu zina nafasi muhimu katika kupunguza umasikini katika nchi za Kiislamu. Amesema kuanzishwa Benki ya Waqfu ni hatua nyingine katika kuwahudumia wanaohitajia nchini Senegal.
805978