Maonyesho hayo yalifunguliwa Ijumaa iliyopita na Mkuu wa Jamaat Islamiya ya Pakistan Sayyid Munawwar Hassan.
Maonyesho hayo yanayofanyika kwa kaulimbiu ya "Soma Qur'ani, Ongoza Dunia" yanajumuisha nakala karibu 500 zilizoandikwa kwa hati za mkono za Qur'ani na tarjumi ya kitabu hicho kwa lugha mbalimbali.
Nakala hizo za Qu'ani zina umri wa karne kadhaa na zimeandikwa kwa hati za wanakaligrafia na maulamaa wakubwa wa ulimwengu wa Kiislamu. Baadhi ya nakala hizo zimeandikwa katika karne za 14 hadi 16.
Maonyesho hayo yanamaliza kazi zake leo. 807023