Kongamano hilo litahudhuriwa na viongozi wa makundi ya kidini kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 25 tangu kiongozi wa zamani wa Kansia Katoliki Papa John Paul wa Pili atoe wito wa kufanyika mkutano wa viongozi wa dini mbalimbali duniani.
Mjumbe wa Papa Benedict wa 16 ambaye amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon Ayatullah Abdul Amir Qabalani amesema kuwa Kongamano la Kimataifa la Mazungmzo kati ya Dini Mbalimbali linafanyika kwa shabaha ya kuwadhihirishia walimwengu kwamba waumini wa dini tofauti wanafanya jitihada za kuimarisha amani, kueneza uadilifu na kushirikiana kwa ajili ya kujenga jamii bora.
Kwa upande wake Ayatullah Qabalani amesisitiza katika mazungumzo hayo juu ya udharura wa kuimarisha ushirikiano kati ya dini za mbinguni katika suala la kuwaongoza wanadamu katika njia ya kheri, amani na ufanisi. 807263