Mkutano huo umewakutanisha viongozi wa Kishia kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Bayt.
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt ni taasisi isiyo ya kiserikali yenye makao yake makuu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Lengo lake ni kueneza mafundisho ya Mtume Mtukufu wa Uislamu na Watu ya Nyumba yake yaani Ahlul Bayt kote duniani.
Kati ya waliohudhuria mkutano huo wa Nairobi ni kiongozi wa Mashia wa Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaki.
807305