Kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Kiutamaduni ya Quds Tukufu Jordan kwa ushirikiano na Jumuiya ya Wahandishi nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Sabil, kongamano hilo limehudhuriwa na wataalamu kadhaa Wapalestina na wasomi 21 kutoka mji mtakatifu wa Quds, Ukingo wa Magharibi na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu. Vilevile washiriki kutoka Saudi Arabia, Imarati, Kuwait, Misri na Algeria wamehudhuria kongamano hilo.
Washiriki wamejadili sera za utawala haramu wa Israel za kuwahamiswa kwa nguvu, kuyahudisha Quds Tukufu na vilevile masaibu ya Wapalestina.
807037