Mtaalamu wa Qur'ani anayeshughulikia uandishi vitabu katika Wizara ya Elimu ya Iran Bw. Reza Nabati amesema mpango maalumu ulianza kwa majaribio mwaka 2009 na sasa utatekelezwa kikamilifu mwaka huu.
Amesema waalimu wa Qur'ani 506 watakaotoa mafunzo hayo wamepita katika kozi maalumu ya kufunza Qur'ani katika shule za msingi. Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha kiwango cha qiraa ya Qur'ani miongoni mwa wanafunzi wa darasa la nne na pia la tano.
807293