IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Malaysia kuanza leo

16:11 - June 13, 2011
Habari ID: 2137625
Mashindano ya 54 ya taifa ya Qur'ani ya Malaysia yanatazamiwa kuanza leo usiku yakihudhuriwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Najib Tun Razzak. Mashindano hayo yanafanyika katika mji wa Kuching katika jimbo la Sarawak.
Shirika la habari la Malaysia Barnama limeripoti kuwa mashindano hayo yatafunguliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo akiandamana na mkewe Rasma Mansour chini ya anwani ya "Malaysia Moja, Umma Mmoja".
Jumuiya ya Ustawi wa Kiislamu ya Malaysia inayosimamia mashindano hayo imetangaza kuwa mashindano hayo yatafanyika katika jengo lenye usanifu majengo unaofafana na ule wa Morocco mjini Sarawak.
Mashindano hayo yataendelea hadi Ijumaa tarehe 17 Juni kwa kutolewa zawadi kwa washindi. Mbali na zawadi za fedha, washindi watapelekwa Makka kutekeleza ibada ya hija na wataiwakilisha Malaysia katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.
Vijana 29 wa kike na kiume kutoka majimbo yote ya Malaysia wanachuana katika mashindano hayo.
Mashindano ya taifa ya Qur'ani ya Malaysia hufanyika kila mwaka kwa shabaha ya kuwashajiisha vijana kusoma Qur'ani Tukufu. 807736

captcha