Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Utamaduni na Masuala ya Kiislamu kinachofungamana na Msikiti wa Abdallah bin al-Hussein.
Washiriki 30 kutoka nchi 27 za Kiarabu na Kiislamu wanashiriki katika makundi tofauti ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani nzima, juzuu 20, juzuu 10 na usomaji pamoja na tafsiri za aya za kitabu hicho kitakatifu.
I'tidal al-Ibadi mkuu wa kitengo cha masuala ya wanawake cha Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan alizungumza jana katika ufunguzi wa mashindano hayo na kusisitiza juu ya umuhimu wa hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur'ani Tukufu na kusema kuwa watu wanaojishughulisha na masuala hayo wana nafasi muhimu mbele ya Mwenyezi Mungu, hapa dunia na huko Akhera. 807714