IQNA

Mashindano ya Qur'ani yafanyika Tanzania

15:33 - June 14, 2011
Habari ID: 2138151
Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Tanzania imenadaa mashindano ya Qur'ani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa idara ya habari ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa, mashindano hayo ya hifdhi na kiraa yalifanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra SA.
Awamu ya mwisho ya mashindano hayo ilifanyika katika hafla iliyodhudhuriwa na Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Dr. Hussein Mwinyi, Balozi wa Iran nchini Tanzania Bw Mohsen Movahhedi Ghomi, Mufti wa Dar-es-Salaam Sheikh Al Hadi Musa Salim na wanazuoni wengine wa Tanzania.
Maustadh wa Qur'ani kutoka Misri na Tanzania walikuwa katika jopo la majaji wa mashindano hayo.
Washindi wawili katika mashindano hayo watawakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran.
807856
captcha