Kampuni ya sauti na picha ya Sautul Qahirah ndiyo itakayotoa CD hiyo ya marehemu Sha'rawi ambayo inakusanya vitabu mbalimbali, tafsiri ya Qur'ani na hutuba zake kuhusu ibada za siku ya Ijumaa.
Kampuni ya Sautul Qahirah pia imepanga kufanya kikao cha kumkumbuka Ustadh Muhammad Sha'rawi siku ya Ijumaa ijayo kwa mnasaba wa kutimia miaka 13 tangu mwanazuoni huyo afariki dunia.
Muhammad Mutawalli al Sha'rawi alizaliwa tarehe 5 Aprili mwaka 1911 katika kijiji cha Daqadus kwenye mkoa wa Dahqaliya nchini Misri na kupata umashuhuri kama mmoja wa wafasiri wa Qur'ani wa zama zake. Mwanazuoni huyo ametoa huduma kubwa kwa Uislamu na umma wa Kiislamu hususan katika medani ya tafsiri ya Qur'ani Tukufu. Alifariki dunia tarehe 17 Juni 1998. 808716