IQNA

Masomo ya Qur'ani kwa wanawake wa Imarati yanaendelea

18:26 - June 14, 2011
Habari ID: 2138340
Masomo ya Qur'ani maalumu kwa wanawake wa Imarati yamekuwa yakiendelea huko mjini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa utayarishaji wa kitengo cha mwongozo cha Idara ya Masuala ya Kiislamu na Kheri ya Dubai.
Masomo hayo ambayo yanafanyika chini ya nara ya 'Dini Yangu, Utambulisho Wangu' yataendelea hadi tarehe 30 Novemba mwaka huu. Masomo hayo ambayo yanafanyika katika fremu ya mpango wa utamaduni wa familia yatajadili masuala mbalimbali yanayohusiana na umuhimu wa wanawake kujifunza Qur'ani Tukufu pamoja na usomaji wake sahihi.
Abdallah Muawwadh, mhubiri wa Kiislamu katika idara kuu ya polisi ya Dubai ni miongozi mwa watu waliopangiwa kutoa hotuba katika vikao mbalimbali vya mpango huo maalumu wa masomo kwa wanawake.
Katika upande wa pili, Iman Ismail Abdullah ambaye ni mkurugenzi mwandamizi wa mpango huo anasema kuwa masomo hayo yaliyoanza tarehe 8 Mei yana lengo la kuwafundisha wanawake wa Imarati mafunzo ya Qur'ani, tafsiri pamoja na usomaji sahihi wa kitabu hicho cha mbinguni. 808524
captcha