Kwa mujibu wa gazeti la Al Qabas, Idara ya Maonyesho ya Kimataifa ya Kuwait itaandaa maonyesho hayo yatakayoendelea hadi Agosti 13.
Rumi Matar Ar Rumi Mkurugenzi wa masuala ya hija amesema maonyesho hayo ni hatua muhimu ya kukutanisha pamoja mashirika na wataalamu wa hija na hivyo kutoa fursa ya kubadilishana mawazo na kustawisha huduma kwa mahujaji nchini humo.
‘Ongezeko la bei, kuchelewa ndege, uchukuzi, ukosefu wa nafasi za kambi katika maeneo ya Mina na Arafat ni kati ya matatizo ya mahujaji ambayo wizara inajaribu kutatua’, ameongeza.
808131