Gazeti la kila siku la Al Arab limeandika katika toleo lake la Juni 13 kuwa Idara ya Takwimu ya Qatar imesema jina la Mtume wa Uislamu Muhammad SAW ndio mashuhuri zaidi miongoni mwa watoto wa kiume huku Fatima jina la bintiye Mtume likiwa mashuhuri zaidi miongoni mwa watoto wa kike.
Kuna watu 14470 raia wa Qatar ambao jina lao ni Muhammad. Abdullah (Jina la baba na mtoto wa Mtume SAW) 8878, Ali 6507, Hamd 5937, na Ahmad 4640 kwa utaratibu kama majina ya wavulana. Majina mengine mashuhuri ni Khalid (3958), Nassir (3428), Abdurrahman (3340), Rashid (3329) na Abdulaziz (3127).
Katika majina ya kike baada ya Fatima (6420), majina mengine mashuhuri ni Maryam (6311), Nurah (6249), Aisha (4359), Sarah (3372), Sheikha (2964), Hiyah (2048), Muzah (1899), Hissah (1881) na Al-Unud (1803).
Qatar ni nchi ya kisiwa kidogo katika Ghuba ya Uajemi yenye idadi ya tatu takribani milioni moja na nusu. Aghalabu ya wanaoishi nchini humo ni watu kutoka Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia na nchi za Kiarabu.
808385