IQNA

Waislamu Ghana watakiwa kuinua kiwango cha elimu

12:39 - June 18, 2011
Habari ID: 2139643
Mtaalamu wa masuala ya elimu wa Ghana Sheikh Dr. Ismaeel Saeed Adam ametoa wito kwa Waislamu nchini humo kutambua kiwango chao cha elimu za kisasa.
Sheikh Adam alikuwa akizungumza Juni 14 katika mji wa Kumasi kusini-kati mwa Ghana wakati wa semina ya ustawi wa vijana walio katika mwaka wa mwisho katika Shule ya Sekondari ya Sakafia.
Amesema kuna haja ya kutatua tatizo kubwa la ukosefu wa kazi, umasikini na kutojua kusoma katika jamii za Waislamu wa eneo hilo.
Sheikh Adam alisema sasa Waislamu wanapaswa kutoa kipaumbele kwa vizingiti vya ustawi wa vijana Waislamu katika zama hizi za utandawazi.
Amewataka vijana Waislamu nchini Ghana wawe wacha Mungu na wazingatie maadili ya kazi ili waweze kufanikiwa maishani.
Ghana ni nchi iliyo magharibi mwa Afrika yenye idadi ya watu takribani milioni 24 na Waislamu ni karibu asilimia 20 ya wakaazi wa nchi hiyo.
809990
captcha