Kwa mujibu wa tovuti ya Marketwire, wawakilishi wa mashirika tofauti ya kiraia yanayounga mkono Wapalestina, waandishi wa magazeti na wanachama wa taasisi za kimataifa kutoka nchini Canada wana lengo la kusafiri kwa meli ya Tahrir mwishoni mwa mwezi huu ili kujiunga na msafara wa 'Uhuru Nambari 2' kwa shabaha ya kuvunja mzingiro huo.
Viongozi wa Kiislamu, Kikristo na Kiyahudi pamoja na wawakilishi wa mirengo ya kisiasa ya Canada pia wanatazamiwa kuwa miongoni mwa wasafiri wa meli hiyo.
Habari zaidi zinasema kuwa wabunge wanne kutoka Ubelgiji, wanne kutoka Australia, watano kutoka Denmark na mbunge mmoja kutoka Ujerumani wanatazamiwa kujiunga na wasafiri wa meli ya Tahrir kwa madhumuni ya kwenda Gaza kuvunja mzingiro huo. 809909