Waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya dunia walianza kumiminika katika Haram ya Imam Hussein jana kwa ajili ya shughuli hiyo iliyofanyika leo.
Misafara ya makundi mbalimbali ya Waislamu wamekumbuka msiba huo wa kufariki dunia Bibi Zainab kwa kuingia katika Haram ya Imam Hussein (as) katika makundi tofauti.
Vyombo vya usalama vya Iraq vimeimarisha ulinzi katika mji huo mtakatifu kwa ajili ya kuwadhaminia usalama Waislamu hao waliokuwa wakiomboleza.
Misafara mingine ya waombolezaji iliingia mjini Karbala ikitokea Najaf kwa ajili ya kukumbuka tukio la kuhuzunisha la kuaga duna binti wa Imam Ali bin Abi Twalib na mjukuu huyo wa Mtume wetu Muhammad (saw).
Shujaa wa Karbala Bibi Zainab binti Ali (as) aliaga dunia tarehe 15 Rajab mwaka 62 Hijria. 810571