Msemaji wa NATO ambaye amekutana na Katibu Mkuu wa OIC amesema Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ni katika wanachama wa kundi la mawasiliano kuhusu Libya na imefanya jitihada kubwa za kidiplomasia na kibinadamu nchini humo.
Amedai kuwa tokea hapo mwanzoni NATO ilianzisha mawasiliano na jumuiya za kieneo na kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
Amedai kuwa mashambulizi ya kijeshi ya NATO yanawalenga mamluki wa utawala wa Muammar Gaddafi kwa ajili ya kuwalinda raia wa Libya!
Madai hayo yanatolewa katika hali ambayo hadi sasa mashambulizi ya NATO yamesababisha vifo vya raia wengi wakiwemo wanamapinduzi wanaopigana kwa lengo la kuondoa madarakani utawala wa Gaddafi. 810319