IQNA

kikao cha darsa ya Qur'ani kufanyika Chuo Kikuu cha London

18:31 - June 18, 2011
Habari ID: 2140104
Kikao cha tafsiri ya baadhi ya sura za Qur'ani Tukufu kitafanyika tarehe 2 Julai katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza.
Prf. Muhammad Abdulhalim na Imam Ahmad Farooq watatoa darsa ya baadhi ya sura za Qur'ani katika kikao hicho kitakachosimamiwa na Akademia ya Sayansi ya Qur'ani ya Britani na Taasisi ya Utafiti na Ustawi wa Kiislamu.
Sura zitakazojadiliwa katika kikao hicho ni Jumua, Munafiqun na Taghabun.
Akademia ya Sayansi ya Qur'ani ya Uingereza pia tarehe 13,14, 20, na 21 za mwezi mtukufu wa Ramadhani itakuwa na warsha ya mafunzo mjini London chini ya anwani ya "Safari ya Ndani ya Qur'ani".
Katika warsha hiyo washiriki watafundishwa maana ya misamiati 1000 iliyotumiwa katika Qur'ani, ujumbe wa kitabu hicho, visa vilivyotajwa ndani yake na masomo ya kitabu hicho kitukufu. 810295

captcha