IQNA

Jarida la Qur’ani na Tiba kuchapishwa Iran

12:05 - June 19, 2011
Habari ID: 2140218
Toleo la kwanza la Jarida la Qur’ani na Tiba litachapishwa na Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Rahim Ghorbani Mkuu wa Kituo cha Etrat katika Wizara ya Afya amesema jarida hilo la kila miezi mitatu litakuwa la kwanza la aina yake ambalo litashughulikia masuala ya utafiti wa Qur’ani na Tiba.
Amesema kamati ya kisayansi imeshabuniwa kwa lengo la kutayarisha toleo la kwanza la jarida hilo. Ghorbani amesema tolea la kwanza litachapishwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mostafa Ghanei ambaye ni mkuu wa utafiti na teknolojia katika Wizara ya Afya ametajwa kuwa mkurugenzi wa jarida hilo huku Mehdi Esfehani akiwa mhariri mkuu.
809311

captcha