Rahim Ghorbani Mkuu wa Kituo cha Etrat katika Wizara ya Afya amesema jarida hilo la kila miezi mitatu litakuwa la kwanza la aina yake ambalo litashughulikia masuala ya utafiti wa Qur’ani na Tiba.
Amesema kamati ya kisayansi imeshabuniwa kwa lengo la kutayarisha toleo la kwanza la jarida hilo. Ghorbani amesema tolea la kwanza litachapishwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mostafa Ghanei ambaye ni mkuu wa utafiti na teknolojia katika Wizara ya Afya ametajwa kuwa mkurugenzi wa jarida hilo huku Mehdi Esfehani akiwa mhariri mkuu.
809311