Hayo yamesemwa na mhadhiri wa Kitivo cha Teolojia cha Chuo Kikuu cha Ferdousi katika mji mtakatifu wa Mas'had huko kaskazini magharibi mwa Iran Bibi Suhaila Piroozfar katika makala iliyopewa anwani ya Uchunguzi katika Maisha na Misingi ya Tafsiri ya Mughnia.
Ameandika kuwa katika tafsiri hiyo Allamah Mughnia anaanza kwa kutoa ufafanuzi kuhusu jina la sura husika idadi ya aya zake, iliteremshwa Makka au Madina na kadhalika na kujadili kauli na mitazamo tofauti ya wanazoni wa tafsiri kuhusu masuala hayo.
Amesema kuwa Allamah Muhammad Jawad Mughnia aliandika tafsiri hiyo akiwalenga zaidi vijana kwa sababu aliamini kuwa mambo kama upendo, udugu, uadilifu, usawa na ukweli ambayo ni misingi muhimu katika dini ya Kiislamu, yamesahauliwa na kizazi cha vijana.
Katika sehemu nyingine ya makala hio, Bi Suhaila Piroozfar amesema Allamah Mughnia alitegemea hadithi zilizopokewa kutoka kwa Ahlul Bait (as) katika kutoa ufafanuzi na tafsiri ya aya za Qur'ani Tukufu.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa tafsiri ya al Kashif imetarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili na taasisi ya Al Itrah Foundation ya Dar es Salaam, Tanzania. 810744