IQNA

Kozi ya Qur'ani ya washichana yafanyika Qatar

15:37 - June 20, 2011
Habari ID: 2141327
Kozi fupi ya kuhifadhi Qur'ani kwa ajili ya washichana inaanza Juni 20 Doha mji mkuu wa Qatar.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Sharq, kozi hiyo ya Qur'ani Tukufu na Misingi ya Tajweed ni ya watoto walio na umri wa kati ya miaka 6-8.
Kozi hiyo ambayo imeandaliwa na Taasisi ya Kuhifadhi Qur'ani ya Al Munir itamalizika baada ya wiki tano.
Taasisi hiyo inapanga kuandaa kozi ya kielimu kuhusu misingi ya tajweed.
Taasisi ya Kuhifadhi Qur'ani ya Al Munir ilibuniwa mwaka 2009 chini ya usimamizi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar. Taasisi hiyo imeandaa kozi 6 za Qur'ani hadi sasa.
810955
captcha