IQNA

Mpango wa miaka 20 wa kuwafunza watoto Qur’ani unahitajika

14:58 - June 22, 2011
Habari ID: 2142257
Masomo ya Qur’ani kwa ajili ya watoto nchini Iran yanapaswa kuratibiwa kwa msingi wa mpango wa miaka 20 na kujumuisha masuala ya kielimu, kifedha na uwezo wa kieneo pamoja na nguvu kazi.
Hayo ni kwa mujibu wa mtaalamu wa Qur’ani na mwalimu Bw. Mahmoud Lotfnia.
Akizungmza na IQNA, amesema hakuna mafanikio yatakayopatikana iwapo vizingiti vilivyopo havitaondolewa. Ametoa wito kwa Wizara ya Elimu ya Iran kusimamia kikamilifu masomo ya Qur’ani ya watoto.
Amesema vituo vyote vya kutoa mafunzo ya Qur’ani kama vile Darul Qur’an vinapaswa kusimamiwa na Wizara ya Elimu ili kuhakikisha kunapatikana mafanikio.
811262
captcha