IQNA

Nigeria kuwa na benki ya kwanza ya Kiislamu

14:29 - June 22, 2011
Habari ID: 2142428
Benki Kuu ya Nigeria Jumatatu iliyopita ilitoa kibali cha kuanzishwa benki ya kwanza ya Kiislamu nchini humo.
Akizungumzia suala hilo katika kikao cha kujadili benki za Kiislamu kinachoendelea sasa huko Dakar, mji mkuu wa Senegal, Sanusi Lamido, Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria amesema kuwa benki hiyo ya kwanza ya Kiislamu itaanzishwa hivi karibuni nchini Nigeria kwa jina la Jaiz. Amesema Nigeria imekuwa ikifanya juhudi za kuanzisha benki ya Kiislamu nchini humo kwa ajili ya kutoa huduma za benki za Kiislamu na kuwa kituo muhimu cha kieneo cha huduma hizo.
Kikao hicho ambacho kinamalizika leo Jumatano huko Senegal kinajadili masuala ya huduma na mfumo wa benki za Kiislamu barani Afrika na hasa katika eneo la magharibi mwa Afrika.
Wakurugenzi na wataalamu wa masuala ya benki na wanazuoni wenye ujuzi katika masuala ya sheria za Kiislamu zinazohusiana na masuala ya kiuchumi na kifedha wanashiriki kwenye kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Wizara ya Fedha na Uchumi ya Senegal. 812727
captcha