IQNA

Iran yasema Marekani ndio mtenda jinai mkubwa dhidi ya binadamu

15:36 - June 23, 2011
Habari ID: 2143143
Kamanda mwandamizi katika majeshi ya Iran amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kwanza kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Marekani kabla ya kuteua mkaguzi maalumu wa haki za binadamu kuhusu Iran.
Naibu Mkuu wa Idara ya Vikosi Vyote vya Majeshi ya Iran Brigedia Jenerali Masoud Jazayeri amesema takwimu zinaonyesha kuwa jinai kubwa zaidi dhidi ya binadamu zinatekelezwa na kuratibiwa Marekani.
Jazayeri amesema kuna makumi ya magereza yaliyoanzishwa kinyume cha sheria nchini Marekani. Aidha amesema huko Marekani kunafanyika vitendo vingi vya utesaji, ukiukaji haki za binadamu, unanyasaji kijinsia dhidi ya raia na ubaguzi wa rangi. Kamanda huyo mwandamizi wa Iran amesema hivi sasa wanajeshi katili wa Marekani wanawaua kinyama raia wa nchi zingine duniani na hata baadhi ya jinai zao hutangazwa katika vyombo vya habari.
Hivi karibuni, kufuatia uchochezi wa Marekani, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilimteua waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Maldives Ahmed Shaheed kuwa mchunguzi wake wa haki za binadamu nchini Iran. Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kuna haja ya kuchunguzwa ukiukwaji wa haki za binaadamu katika nchi za Magharibi.
813614
captcha