IQNA

Iran kuandaa maonyesho ya Qur'ani Sudan

15:35 - June 23, 2011
Habari ID: 2143144
Waziri wa Utamaduni wa Sudan Al-Samawal Khalfallah na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran Dr. Seyyed Mohammad Hosseini wametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaandaa maonyesho ya Qur'ani na kuanzisha kitengo cha Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu nchini Sudan.
Katika mkutano uliofanyika Tehran Juni 19 mawaziri hao wawili walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili za Kiislamu. Dr. Hosseini ameashiria mapambano ya viongozi wa Sudan na Iran dhidi ya mabeberu wa dunia na kusema nchi hizi mbili zina mitazamo sawa katika uga wa kimataifa. Ameelezea matumaini yake kuwa Iran na Sudan zitaimarisha zaidi ushirikiano wa kisiasa na kiutamaduni.
Katika mkutano huo Waziri wa Utamaduni wa sudan amesema Tamasha la Utamaduni wa Kitaifa wa Sudan litafanyika mwaka 2011 katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha amewaalika malenga Wairani kushiriki katika tamasha za kiutamaduni nchini Sudan.
811269
captcha