IQNA

Hatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran:

Harakati za wananchi zitapa ushindi

11:33 - June 25, 2011
Habari ID: 2143413
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa harakati za wananchi katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika zitapata ushindi. Ayatullah Muhammad Imami Kashani ameashiria mwamko wa Kiislamu katika nchi mbalimbali na kukosoa ukandamizaji unaofanywa na serikali za nchi hizo.
Amesema kuwa mwamko huu wa Kiislamu hauwezi kuzimwa kwa kukandamiza wananchi.
Akihutubia halaiki kubwa ya waumini katika Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Kashani amesema kuna udharura wa wananchi wa maeneo hayo kupewa haki zao na kutekelezewa uadilifu. Amesema madikteta wa nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika wamepata hasara kutokana na mwamko ulioko wa Kiislamu. Amesisitiza juu ya umuhimu wa kuwepo uadilifu na misimamo ya wastani. Khatibu wa sala ya Ijumaa Tehran ameashiria nara za Kiislamu za wananchi wanamapinduzi wa maeneo hayo na kusema, mataifa ambayo humtegemea Mwenyezi Mungu ndiyo yatakayopata ushindi.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Ayatullah Kashani amemkumbuka shahidi Ayatullah Dkt. Muhammad Beheshti mkuu wa zamani wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran ambaye akiwa pamoja na wenzake 72 waliuawa shahidi katika tukio la kusikitisha la Juni 28 mwaka 1981 baada ya kundi la MKO kutega bomu katika makao makuu yao. Ameashiria Wiki ya Vyombo vya Mahakama ambayo huadhimishwa nchini Iran kwa mnasaba wa tukio hilo na kusema kuna ulazima wa kuzingatia misimamo ya wastani na kujiepusha na misimamo ya kufurutu mipaka katika vyombo vya mahakama.
814170
captcha