IQNA

Barua ya Erdogan kwa Ayatullah Sistani kuhusu hali ya Bahrain

12:13 - June 25, 2011
Habari ID: 2143774
Racep Tayyib Erdogan, Waziri Mkuu wa Uturuki amemwandikia barua Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani, mar'ja mashuri wa Iraq kuhusiana na hali ya mgogoro wa Bahrain na hatua ya utawala wa nchi hiyo ya kuwakandamiza wanamapinduzi kwa ushirikiano wa askari jeshi wa Saudi Arabia.
Barua hiyo ilikabidhiwa kwa mwanazuoni huyo na ujumbe wa Uturuki uliotembelea ofisi yake hapo siku ya Alkhamisi. Katika barua hiyo Waziri MKuu wa Uturuki alichambua kwa ufupi matukio ya eneo la Mashariki ya Kati na hasa ya Bahrain ambako wananchi wa nchi hiyo wanaendesha mapambano dhidi ya utawala wa Aal Khalifa.
Inasemekana kuwa katika mazungumzo yake na ujumbe huo, Ayatullah Sistani amelaani mauaji na jinai za kutisha zinazofanywa na jeshi la Bahrain na Saudi Arabia dhidi ya wananchi wanaopigania haki zao kwa njia ya amani. Amewataka watawala wa nchi mbili hizo kusimamisha mara moja ukandamizaji na mauaji hayo dhidi ya wananchi wasio na hatia.
Huku akilaani uingiliaji wa kijeshi wa kigeni katika mambo ya ndani ya Bahrain, Waziri Mkuu wa Uturuki amefananisha matukio ya Bahrain na tukio chungu katika historia ya Kiislamu la Karbala na kuongeza kuwa Waislamu hawataki kushuhudia tukio jingine kama hilo huko Bahrain. 814155
captcha