Sheikh Ishaq Nuamah, mwandishi na msomi wa Kiislamu amezindua kitabu chenye anwani ya, ‘Haja ya Uhandisi Mpya wa Kijamii wa Vjana Waislamu nchini Ghana’.
Kitabu hicho kimeandikwa na Hajj Zagoon Sayeed Haruna mtaalamu wa masuala ya ustawi wa vijana mwenye makao yake nchini Uingereza. Kitabu hicho kinalenga kutambua na kujadili masuala ya kimsingi yanayowahusu vijana Waislamu.
Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu hicho katika mji mkuu wa Ghana Accra, Sheikh Nuamah amesema kunahitajika mbinu za kitaalamu ili kuwahusisha vijana Waislamu katika maendeleo ya kitaifa. Amesema iwapo vijana Waislamu watahusishwa na maendeleo basi imani yao kwa Mwenyezi Mungu itaimarika. Amewataka vijana wa Ghana kuwa na fahari kwa ajili ya utambulisho wao wa Kiislamu.
Naye Dr. Rabiatu Ammah Konney wa Chuo Kikuu cha Ghana amesema kitabu hicho chenye kurasa 167 kinawaonyesha Waislamu namna wanavyopaswa kulipa umuhimu suala la elimu. 813632