IQNA

Ustadh Tarouti:

Ustadh Shoaisha amekamilisha mbinu ya kiraa ya marehemu Rif'at

10:45 - June 27, 2011
Habari ID: 2145026
Ustadh Abulainain Shoaisha alivutiwa sana na marehemu Muhammad Rif'at, gwiji wa makarii wa Misri na alikamilisha kiraa yake kwa kujaribu kuiga mbinu yake ya usomaji Qur'ani.
Hayo yamesemwa na Ustadh Abdul Fattah Ali Tarouti, karii mashuhuri wa Kimisri katika mahojiano yake na shirika la habari la IQNA. Ameongeza kuwa Ustadh Abulainain Shoaisha alikuwa miongoni mwa wasomaji wakubwa wa Qur'ani na nyota zinazong'ara katika anga ya kiraa nchini Misri na katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesema msomaji huyo aliwaathiri wasomaji wengi wa Qur'ani na sauti yake inazivutia nyoyo za wasikilizaji.
Ustadh Tarouti amesema Sheikh Shoaisha alijifunza katika skuli ya Ustadh Rif'at na aliathiriwa sana na mbinu yake ya usomaji. Ameongeza kuwa akhlaki na maadili ya Ustadh Shoaisha yalikuwa maadili ya Qur'ani.
Jaji huyo wa kimataifa wa Qur'ani amesema kuwa sauti ya Ustadh Shoaisha ilikuwa na mvuto makhsusi wa kimaanawi na alipitisha kipindi kikubwa cha umri wake katika kuhudumia Qur'ani Tukufu.
Akielezea sifa zake za kimaadili, Ustadh Taruti amesema: "Japokuwa Sheikh Shoaisha alikuwa mkubwa zaidi kwetu kiumri lakini alikuwa akiamiliana na watu wote kwa unyenyekevu na heshima kubwa kwa kadiri kwamba tulikuwa hatuhisi tofauti ya kiumri baina yetu na yeye."
Gwiji la wasomaji Qur'ani wa Misri Sheikh Abulainain Shoaisha ambaye alikuwa pia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Makarii na Mahafidh wa Misri alifariki dunia Alkhamisi iliyopita katika hospitali moja mjini Cairo akiwa na umri wa miaka 89. 815464
captcha