Karii mashuhuri ya Misri Abdul Fattah Tarouti pamoja na makarii kadhaa wa kimataifa Wairani watahudhuria vikao hivyo ambavyo vimeandaliwa na Shirika la Waqfu la Iran katika maeneo kadhaa matakatifu mjini Tehran.
Kwa mujibu wa Shirika la Waqfu vikao hivyo vya kusoma Qur’ani vitafanyika katika Haram ya Imamzadeh Hassan (AS) katika Barabara ya Qazvin, Imamzadeh Hadi (AS) katika Shariar, Imamzadeh Saleh (AS) eneo la Tajrish, Imazadeh Aqil (AS) huko Islamshahr, na Imamzadeh Emadeddin (AS) huko Robatkarim.
Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yataanza Juni 29 mjini Tehran na kuendelea hadi Juni 4.
815343