IQNA

Kazakhstan tayari kuandaa mkutano wa OIC

10:57 - June 27, 2011
Habari ID: 2145031
Huku Kazakhstan ikijitayarisha kuandaa kikao cha 38 cha Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC kuanzia Juni 28-30 katika mji mkuu Astana, Rais Nursultan Nazarbayev amejadili umuhimu wa mkutano huo kwa nchi hiyo ya Kiislamu.
‘Kama kiongozi wa taifa jipya ambalo linaadhimisha mwaka wa 20 wa uhuru wake, natoa wito kwa viongozi wa dunia kufanya mazungumzo ya wazi na kushirikiana katika kutafuta njia za kuimarisha usalama na amani duniani’ amesema Nazarbayev katika makala maalumu ya Jarida la OIC.
Ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka hisia dhidi ya Uislamu duniani na kusema hili ni dhihirisho la kutovumiliana, jambo ambalo ni hatari kwa usalama na amani duniani.
Ameutaja ubaguzi dhidi ya Waislamu kuwa mi hatari katika sekta za ajira na nyumba katika baadhi ya nchi nje ya Ulimwengu wa Kiislamu. ‘Tunalaani viitendo vya kuwahujumu na kuwatusi Waislamu katika nchi hizo’, amesema.
Rais wa Kazakhstan ameashiria mwamko wa Kiislamu katika nchi za kiarabu na kusema: ‘Mabadiliko ya kisiasa Tunisia na Misri na maafa ya kibinadamu nchini Libya yamepelekea kujitokeza wimbi kubwa la wakimbizi’.
Amesema matukio hayo yameibua changamoto katika nchi zingine za OIC na kuonya kuwa huenda nchi kadhaa za Kiislamu zikapata hasara kutokana na migororo ya kisiasa.
815440
captcha