Kikao hicho ambacho kitaongozwa na Muhammad Mahmoud Tablawi mmoja wa makarii mashuhuri wa Misri, kitafanyika kwa lengo la kuteua Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Makarii na Mahafidhi wa Qur'ani wa Misri ambaye atachukua nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Sheikh Shoaisha.
Sheikh Muhammad Tablawi amesema kuwa miongoni mwa ajenda za kikao hicho ni kuweka wazi siasa na sera za Baraza la Uendeshaji la jumuiya hiyo. Ameongeza kuwa kikao hicho pia kitabuni mipango ya kudumisha kazi za Sheikh Shoaisha na kukamilisha njia yake.
Gwiji la wasomaji Qur'ani wa Misri Sheikh Shoaisha alifariki dunia Alkhamisi iliyopita mjini Cairo akiwa na umri wa miaka 89. 816058