Katibu Mkuu wa OIC Ekmeleddin Ihsanoglu ameyasema hayo alipozungumza na waandishi habari mjini Astana Juni 27.
'Kesho jumuiya yetu itakuwa na jina jipya na nembo mpya, amewaambia waandishi habari baada ya kumaliza mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kazakhstan Yerzhan Kazykhanov.
Kikao hicho cha OIC pia kitajadili masuala ya mwamko wa Kiislamu katika nchi za Afrika na vilevile masuala ya bara Afrika na hasa Somalia, kadhia ya Afghanistan na masuala ya maeneo mengine duniani, amesema Ihsanoglu.
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ilianzishwa mjini Rabat Morocco mwaka 1969 na ina wanachama 57 na idadi ya watu takribani bilioni 1.2.
816245