Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yalifanyika katika Msikiti Mkuu wa mji mkuu Bishkek.
Mashindano hayo ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yameandaliwa na Idara ya Masuala ya Waislamu nchini Kyrgyzstan.
Mashindano hayo ya kila mwaka ya hifdhi huwa katika vitengo vitatu vya kuhifadhi Juzuu 10, kuhifadhi Juzuu 20 na kuhifadhi Qur'ani kamili.
Mwaka huu vijana 42 walifuzu kufika fainali. 11 walishindana kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 12 Juzuu 20, juzuu 19 na Juzuu 10.
Kyrgyzstan ni nchi iliyo katika eneo la Asia ya Kati ambapo asilimia 86 ya watu wa nchi hiyo ni Waislamu.
814221